23 Novemba 2025 - 20:51
Mamdani: “Trump ni Mfasisti na Mwimla” — Asema Meya Mteule wa New York.Amesema bado ataendelea kuwa wazi, mkosoaji pale inapobidi, na mshirika pale ku

Kwa maneno yake: “Haki na ukweli huwa vinang’aa daima; uongo haudumu.”

Shirika Ia Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Meya mteule wa jiji la New York, Mamdani, amesema kuwa licha ya tofauti kubwa za kisiasa na kiitikadi, mkutano wake wa Ijumaa na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ulikuwa fursa muhimu ya kujadili masuala yanayogusa moja kwa moja maisha ya wakazi wa jiji hilo.

Akinukuliwa akizungumza na vyombo vya habari, Mamdani aliweka wazi mtazamo wake kuhusu Trump kwa kusema: “Rais Trump ni mtu mwenye hulka za ufashisti na uimla. Hata hivyo, kikao chetu kilikuwa nafasi ya kutafuta namna ya kupunguza gharama za maisha kwa wakaazi wa New York.”

Amesema kwamba pamoja na kutofautiana naye kimisimamo, majadiliano ya moja kwa moja na viongozi wa ngazi ya juu ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha kuwa masuala ya msingi kama makazi, usafiri, na huduma za kijamii yanapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Mamdani alisisitiza kuwa kipaumbele chake ni kulinda maslahi ya wananchi, na kwamba ukweli kuhusu mwenendo wa kisiasa wa Trump hauwezi kuficha haja ya kufanya mazungumzo yenye matokeo chanya kwa watu anaowaongoza.

Kwa maneno yake: “Haki na ukweli huwa vinang’aa daima; uongo haudumu.”

Amesema bado ataendelea kuwa wazi, mkosoaji pale inapobidi, na mshirika pale kunapohitajika kwa ajili ya ustawi wa wakazi wa New York.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha